Aliyekua DED Mafia Kassim Ndumbo Aachiwa huru na Mahakama
MAHAKAMA ya Wilaya ya Mafia imemuachia huru mshtakiwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, Ndugu Kassim Seif Ndumbo baada ya kukosekana ushahidi kufuatia Kesi ya Jinai namba 15768/2024 iliyokuwa ikimkabili.
Mahakama imechukua maamuzi hayo baada ya kukosekana shahidi wa mwenendo mzima wa upande wa mashtaka kwenye shauri hilo.
Maamuzi hayo yamekuja baada ya kusikiliza ushahidi kwa upande wa Jamhuri ambao ulikuwa na mashahidi sita kumaliza kutoa ushahidi wao pasipo muhanga(victim) ambaye ilidaiwa kuwa alibakwa.
Imefahamika kuwa, mlalamikaji wa shauri hilo hakuwa muhanga mwenyewe bali ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Mafia, hivyo kwa muda wote wa kusikiliza shauri, hakukuwa na mzazi, ndugu wala muhanga ambaye aliwahi fika mahakamani.
Upande wa Jamhuri ulitoa taarifa ya kutaka kuingiza maelezo ya muhanga kwenye file kwa madai kwamba wameshindwa kumpata muhanga( victim) wa tukio la ubakaji.
Baada ya kusikiliza hoja kwa pande zote mbili, mahakama ilikataa ombi hilo na kutupilia mbali shauri hilo kwa sababu upande wa Jamhuri hawakufanya hatua zozote stahiki za kumpata na kumpeleka muhanga mahakamani kama shahidi muhimu; ambaye kwa ushahidi wa mwenyekiti wa serikali ya kijiji, muhanga huyo ni mke wa mtu anayeishi Lushoto, Tanga
Mwisho.
No comments