Treni ya Mwendokasi (SGR) Kuanza safari kutoka Dar es salaam Kwenda Dodoma July 25
Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa safari ya Treni ya Mwendo kasi ( SGR) kutoka Dar es Salaam mpaka Dodoma inatarajiwa kuanza tarehe 25 Mwezi wa Saba Mwaka Huu,
Mbarawa amesema hayo baada ya kufanya ziara ya kukagua miundombinu ya Reli ya Kisasa SGR kipande cha Dar es Salaam na kujiridhisha kuwa treni hiyo itaanza kuwa maandalizi yanaendelea zivuri.
“ Nimekagua Miundombinu ya madaraja na vivuko pamoja na treni kazi inakwenda vizuri na julai 25,2024 tunatarajia kuanza safari ya Dar es Salaam mpaka Dodoma ‘Alisema Mbarawa.
Pia Waziri Mbarawa amesema kuwa nauli ya treni hiyo itakuwa Rafiki kwa kila Mtanzania ataweza kusafairi kuanzia daraja la kwanza mpaka Daraja la tatu Makame Mbarawa
Katika kuhakikisha safari ya Treni hiyo inaanza bila kuwepo changamoto , Mbarawa amesema kuwa kwa kuanzia mwezi juni Treni hiyo itaanza safari ya Dar es Salaam mpaka Morogoro na mifumo ya tiketi itakuwa tayari na kutoa wito kwa watanzania kuanza kusafiri kwa treni hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amesema kuwa kivuko vya Magari na vya kutembea kwa miguu vitakamailika mapema mwezi ujao na wataongea vivuko vingine vya watembea kwa miguu pale itakapo hitajika
No comments