Header Ads

Header ADS

Red Arrows Ya Zambia Yatwaa Ubingwa wa Kombe la Kagame


TIMU ya Red Arrows ya Zambia imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame kwa ushindi wa penalti 10-9 dhidi ya APR ya Rwanda kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 Leo Uwanja wa Manispaa ya Kinondoni (KMC) Jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji Ricky Banda alianza kuifungia Red Arrows dakika ya 62, kabla ya mshambuliaji wa Kimataifa wa Mauritania kuisawazishia APR dakika ya 90.

Na kwenye mikwaju ya penalti ikawa bahati ya waalikwa kutoka ukanda wa Kusini kwa Afrika (COSAFA) kutwaa taji la michuano hiyo iliyodhaminiwa na Mamlaka ya Bandari Dar es Salaam.

Mapema mchana katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu Al Hilal Omdurman ilishinda kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya dhidi ya Hay Al Wad Nyala, zote za Sudan hapo hapo Uwanja wa KMC.

No comments

Powered by Blogger.