Header Ads

Header ADS

Uongozi Wa Yanga Waweka Wazi Majukumu Ya Chama

Uongozi Wa Yanga Waweka Wazi Majukumu Ya Chama
Clatous Chama

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kiungo wao Clatous Chama amesema ana jambo lake ndani ya majukumu yake mapya msimu wa 2024/25.
Chama ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa Yanga ilikuwa Julai Mosi 2024 msimu wa 2023/24 alikuwa kwa watani zao wa jadi Simba.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa kiungo huyo amekabidhiwa jezi namba 17 kwa mpango kazi maalumu kuendelea kutimiza majukumu yake kwa umakini.
“Chama amekabidhiwa jezi namba 17 kutoka kwa Farid Mussa hii ni kazi nyingine kwake kwa ajili ya kutimiza majukumu yake na tunataka wale wasimsahau haraka wakimuona uwanjani.
“Chama ni yuleyule, uwezo wake ni uleule na amesema kuwa ana jambo lake hivyo ni jambo la kusubiria namna gani itakuwa kikubwa ni kuwa na subira.”

No comments

Powered by Blogger.