Historia kwa kifupi jinsi Uislam ulivyoingia Miono na nani aliuleta
Kutoka Miono Fahamu jinsi uislam ulivyoingia na hadi hii leo Miono kuwa na idadi kubwa ya waislam kuliko wasiokuwa waislam.
Anasimulia CHIEF KOLWA kuwa Shekh Juma Mwenkulo ndiye shekhe wa kwanza kuwa Imamu wa Msikiti wa Stendi Ulipoanzishwa katika kijiji cha miono kilichopo wilaya ya bagamoyo mkoani pwani, Tanzania.
Mashekhe hao wote waliotajwa hapo juu ni miongoni mwa wanafunzi wa kwanza kabisa wa Shekh Salum Kibwana Mganga ambaye ndiye alieuleta uislaam katika kijiji cha Miono.
MSIKITI WA WAGENI.
Msikiti wa Stend uliitwa ni msikiti wa wageni kwa wakati huo kwasababu waarabu waliomba kwa wazee wa mji wa miono wapatiwe eneo wajenge msikiti, Ndio Mzee Ally Kilo (MAKUPILA) Akawapatia eneo lile la Stend, mashekhe wengine wa msikiti huu ni shekhe Jafari Mchuka na Shekhe Maine (Dara).Mashekhe hao wote waliotajwa hapo juu ni miongoni mwa wanafunzi wa kwanza kabisa wa Shekh Salum Kibwana Mganga ambaye ndiye alieuleta uislaam katika kijiji cha Miono.
Kwasasa walioshika nafasi hizo za mashekhe waasisi wa Uislam Miono ni kama ifuatavyo hapa chini
1.) Shekhe Mkuu Salum Kibwana (HOZA) kwasasa amechukua Shekh Iddi Ramadhani (ZARAU)
2.) Nafasi ya shekhe wa Miono Maine (DARA) Amechukuwa shekh Amiri Mohamed ndio wanaoendeleza uislam kwa nafasi zao walioridhiwa na waislam Miono
Ikumbukwe kuwa kabla ya Ujio wa Shekhe Salum Kibwana Miono yote walikuwa wapagani wakifuata mila za jadi
HIO NDIO HISTORIA FUPI YA KUINGIA KWA UISLAM MIONO.
Chanzo:
(((((((CHIEF KOLWA))))))))))
Ikumbukwe kuwa kabla ya Ujio wa Shekhe Salum Kibwana Miono yote walikuwa wapagani wakifuata mila za jadi
HIO NDIO HISTORIA FUPI YA KUINGIA KWA UISLAM MIONO.
Chanzo:
(((((((CHIEF KOLWA))))))))))
No comments