Header Ads

Header ADS

Kibindu Tunayoitaka watekeleza Ahadi Yao Kuchangia ujenzi wa Darasa Miono

Kibindu Tunayoitaka watekeleza Ahadi Yao Kuchangia ujenzi wa Darasa Miono
Mwenye Tshirt ya Blue bahari ni Mwakirishi wa wana Kibindu tunayoitaka


Historia kwa ufupiWana Miono wazawa waishio Miono, nje ya Miono na hata waishio nje ya Nchi ya Tanzania waliunda group la WhatsApp linalojulikana kwa jina la Kukaya Miono Likiwa na maana ya “Nyumbani Miono” ililoanzishwa tarehe 06/12/2023, Mnamo tarehe 10/02/2024 walizindua rasmi ujenzi wa darasa katika shule ya msingi Miono ikiwa ni miongoni mwa Malengo ya Group hili Bofya hapa kusoma

Siku hiyo ya uzinduzi mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi isio ya kiserikali ya TETE Foundation Bi. Susan Senso. Pia walihudhuria wana Kibindu tunayoitaka, ambao wali ahidi kuchangia tofali 100 na huenda zikazidi.

Unaweza kutazama video hapo chini ya wana Kibindu Tunayoitaka wakiahidi kuunga mkono jitihada za wana Kukaya Miono za kujenga darasa shule msingi miono


Utekelezaji wa Ahadi yaoBaada ya kuahidi katika siku hii ya uzinduzi wa ujenzi wa darasa walianzisha harembee za kuchangishana pesa kwaajili kuchangia tofali 100 walizo ahidi.

Mpaka kufikia Tarehe 24/03/2024 Umoja huu ulikabidhi kiasi cha shilingi laki moja elfu themanini na mbili na mia sita 182,600/=

Je na wewe umevutiwa na ungependa kuchangia jitihada hizi za wananchi wa Miono kuleta maendeleo katika Kijiji chao.


Tuma mchango wako kwa Admin Mkuu namba hii 0785 429 686 Jina Omari Mtiga

No comments

Powered by Blogger.