Header Ads

Header ADS

Darasa la bure: Kanuni na ulimaji bora wa zao la Muhogo 2024

Darasa la bure: Kanuni na ulimaji bora wa zao la Muhogo 2024
Picha ya zao la muhogo shambani

Misingi na kanuni za kilimo bora. Neno Msingi lina maana ya mwanzo wa kufanya shughuli yeyote inayokusudiwa ili kuweza kufikia malengo, kwa hiyo katika kilimo ipo misingi muhimu ifuatayo:

Kuwa na mipango thabiti inayotekelezeka kabla ya kuanza kufanya kazi yeyote ya maendeleo ni vyema kuweka mpango kazi ili iwe dira wakati wa utekelezaji. Hivyo wakulima wanatakiwa waweke malengo yao ya kilimo kwa kuangalia usalama wa chakula na kipato 

Mipango bora. 

Ni mipango ambayo inamsaidia mkulima kupata chakula cha kutosha na fedha ili kuondokana na umaskini. Mipango inatakiwa iwe shirikishi kwa kuona kuwa wakulima wana shiriki katika kupanga, kutekeleza, kufuatilia pamoja na kutathmini. 

Kuchagua eneo linalofaa kwa kilimo. 

Kwa kuwa kilimo ni kazi ya kisayansi, eneo linalofaa kwa kilimo liwe na rutuba, mteremko wa wastani, liwe sehemu inayopitika ili kurahisisha usafirishaji wa mazao na pembejeo wakati wa uzalishaji. 

Uwekaji na utunzaji wa kumbukumbu. 

Ni muhimu mkulima kujiwekea kumbukumbu za uzalishaji, mapato na faida ili kupima mafanikio ya kazi yake. 

Matumizi ya kanuni za kilimo bora. 

Neno kanuni lina maana ya utaratibu wa kisanyansi uliofanyiwa majaribio kwa muda mrefu na ambao umekubalika utumike wakati wa uzalishaji wa mazao. Kanuni za kilimo bora 
  •  Kutayarisha shamba mapema Kwa kutifua. 
  •  Kupanda mbegu bora kwa nafasi inayostahili. 
  •  Kupunguzia miche na kubakiza inayoshauriwa 
  •  Palilia mapema-si zaidi ya wiki mbili baada ya kuota mazao..Plazi ziwe mbili au zaidi. 
  •  Weka mbolea ya kukuzia mara baada ya palizi. 
  •  Weka dawa ya kuua wadudu wa mimea. 
  •  Linda mazao yako na Wanyama waharibifu 
  •  Vuna mazao yako baada ya kukomaa vizuri. 
  •  Sindika mazao yako na kuyaweka kwenye mifuko inayoingiza hewa baada ya kuweka dawa. 
  •  Hifadhi mazao mahali pazuri pasipo vuja au kufikiwa na wanyama waharibifu.( Panya) 
Darasa la bure: Kanuni na ulimaji bora wa zao la Muhogo 2024
Muhogo ukiwa tayari uko sokoni

Zao la muhogo 
Utangulizi 

Zao la mihogo ni muhimu hapa wilayani na huzalishwa karibu katika kata zote. Hata hivyo wakulima wengi bado wanatumia mbegu za asili ambazo hutoa mavuno kidogo. Jitihada zinafanywa za kusisitiza matumizi ya aina ya kisasa hususan Kiroba ambayo inaukinzani na ugonjwa wa mihogo uitwao batobato. Faida ya zao hili ni kwamba hustahmili ukame, mizizi, miti na majani hutumika kwa chakula mbegu na mboga, pia huweza kukaa ardhini kwa muda mrefu bila kuharibika 

Aina za mihogo 

Zipo aina mbali mbali za mihogo za asili lakini kwa sasa inashauriwa kutumia aina za kisasa ambazo ni: Kiroba na Msitu Zanzibari kwa sababu hukomaa haraka na kutoa mazao mengi. Pia Kiroba inaukinzani na ugonjwa wa batobato wa mihogo. 

Utayarishaji wa shamba 

Shamba la mihogo ni vema litayarishwe mapema kwa kukata miti, vichaka kisha tifua vizuri kiasi ya sm 15 hadi 30. Aidha shamba linaweza kutayarishwa kwa kutumia matuta. 

Upandaji na nafasi za kupandia 

Mihogo hupandwapingili zilizochaguliwa kutoka katika mimea iliyokomaa vizuri na isiyo na ugonjwa. Pingili hukatwa kwa kisu kwa urefu wa sm 30 hadi 45 tayari kwa kupelekwa shamba ili zipandwe. Mihogo hupandwa kwa nafasi ya sm 120x90 kwenye shamba la sesa na sm 150x75 kwenye shamba la matuta. Sio muhimu kutumia mbolea za kupandia za viwandani isipokuwa iwapo shamba halina rutuba inashauriwa kutuima samadi kiasi cha tani 4 hadi 5 kwa eka. 

Palizi 

Palizi huanza baada ya wiki mbili toka kupandwa na jembe la mkono hutumika na kurudia mara kwa mara mpaka mihogo inapokomaa. Hakuna haja ya kupunguza miche kwa sababu hupndwa pingili moja kwa shina. 

Mbolea za kukuzia 

Mbolea za viwandani sio muhimu kwa zao la muhogo. 

Dhibiti ya wadudu 

Wadudu wanaothiri mihogo ni mchwa, vidugamba na inashauriwa kutumia dawa aina ya Karate au Decis kiasi cha cc125 kwa lita 20 za maji. 

Magonjwa 

Mihogo huathiriwa zaidi na ugonjwa wa bato bato kali kwenye majani pamoja na ule wa kuoza mizizi. Magonjwa haya hukingwa kwa kunda mbegu ambazo hazina ugonjwa au kutumia aina ya mihogo yenye ukinzani ambayo ni Kiroba. Pia inshauriwa kutumia kanuni za kilimo bora ili kupunguza athari ya magonjwa haya. 

Ukomaaji na uvunaji 

Mihogo hukomaa baada ya miezi 12 had 18 kutegemea na aina ya mihogo, hali ya hewa pamoja na utunzaji. Mihogo iliyokomaa ivunwe kwa kungoa mashina na eka moja iliyotunzwa vizuri hutoa tani 4 hadi 10. 

Hifadhi na uuzaji 

Mihogo iliyovunwa humenywa na kukaushwa juan ili kauke vizuri. Mihogo iliyokaushwa husagwa unga na kuuzwa au huhifadhiwa kama makopa kwa matumizi ya baadae

No comments

Powered by Blogger.