Header Ads

Header ADS

Mahakama ya Hakimu mkazi kisutu yatengua uraisi wa Mhandisi Hersi Said Yanga

Engeneer: Hersi Saidi
Kutoka katika chanzo cha kuaminika cha Millard Ayo kimeripoti taarifa ifuatayo inayomuhusu Raisi wa klabu ya timu ya yanga Mhandisi Hersi Saidi.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam, imeamuru Uongozi wa Club ya Yanga ukiongozwa na Rais wa Yanga Injinia Hersi Saidi na wenzake, kuachia ngazi na kuondoka kwenye Club hiyo kwakuwa Katiba ya Yanga haitambui uwepo wao.

Imedaiwa kuwa uamuzi huu wa Mahakama umekuja baada ya Kundi la Wazee wachache waliowahi kuwa Wazee wa Yanga kipindi cha nyuma, kushitaki Mahakamani likidai uwepo wa Viongozi wa sasa wa Yanga (Injinia Hersi na wenzake) ni batili na haujafuata Katiba ya Club hiyo.

Kutokana na Wazee hao kushinda kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, inamaana kuwa Rais wa Yanga Injinia Hersi na Viongozi wenzake wanatakiwa kuachia ngazi na kukabidhi Ofisi kuanzia sasa.

Injinia Hersi alianza kuiongoza Yanga kama Rais miaka miwili iliyopita baada ya kushinda nafasi hiyo akiwa ni Mgombea pekee July 2022 na kumfanya kuwa Rais wa kwanza wa Yanga SC toka kuanza kwa mfumo mpya wa mabadiliko ambapo alitangazwa kuwa atakuwa madarakani kwa miaka minne ( hadi 2026 ) kwa mujibu wa Katiba ya Club

No comments

Powered by Blogger.