Header Ads

Header ADS

ZANZIBAR MAPUMZIKO MWAKA MPYA WA KIISLAM 1446H KESHO JUMATATU

ZANZIBAR MAPUMZIKO MWAKA MPYA WA KIISLAM 1446H KESHO JUMATATU

Zanzibar itaadhimisha Mwaka mpya wa Kiislam 1446 Hijiriya na kesho Jumatatu sawa na mwezi 1 Muharram 1446 Hijiriyya sawa na tarehe 08/07/2024 Miladia. Huu ni mwaka wa pili sasa tangu kutangazwa kwa mapumziko hayo na sikukuu ya Mpya wa Kiislam mnamo mwaka jana 2023 na kutangazwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi @dr.hmwinyi .

Dk Hussein Mwinyi alisema hayo Julai 31, 2022 katika kongamano lililofanyika msikiti wa Jamiu Zanzubar, Mazizini, mkoa wa Mjini Magharibi.

Rais Mwinyi alisema maadhimisho hayo yatafanyika kwa mzunguko kati ya Unguja na Pemba ili kutoa nafasi kwa waislamu kushiriki. Alisema utaratibu wa kuadhimisha mwaka mpya wa kiislamu utawasaidia waislamu kuujua mwaka wao kidini.

Waislamu wanatumia Kalenda ya Hijiri ambayo miezi yake huanza na kuisha kulingana na mbalamwezi. Kutoweka kwa mwezi kunaashiria mwisho wa mwezi. Kalenda hii iliundwa rasmi mwaka 622AD wakati wa utawala wa Khalifa Umar ibn al-Khattab. Kalenda hii inatumika kuashiria matukio na tarehe muhimu za kiislamu kama vile Ramadhani, Eid al-Fitr, Eid al-Adha na mwanzo wa msimu wa Hija.

Mwaka wa Hijiri una miezi kumi na miwili; Muharram, Safar, Rabi’Al-Awal, Rabee’Al-Akhir, Jumada Al Ula, Jumada Al-Akhirah, Rajab, Shaabani, Ramadhani, Shawwal, Dhu Al Qa’da na Dhu Al Hijja.

Chanzo: @miladu_tv

No comments

Powered by Blogger.