Video: Mwanasheria Wa Yanga Atoa Tamko Zito Kuhusu Magoma Na Wenzake
Simon Patrick – Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga.
Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga, Simon Patrick amesema wamegundua Walalamikaji Juma Ally na Geofrey Mwaipopo waliofungua kesi wakitaka Rais wa klabu hiyo Eng.Hersi Said na viongozi wengine waachie ngazi, kuna Watu wapo nyuma yao na wanatumika kuleta vurugu ambapo kwa kushirikiana na vyombo vya usalama, Yanga imeanza kufanya uchunguzi ili kuwabaini walio nyuma yao.

Akiongea leo Julai 17,2024 Jijini Dar es salaam, Simon amesema “Mnamo tarehe 6/11/2022 watu wawili waliojiita Wanachama wa Young Africans SC walifungua kesi Mahakama ya Kisutu, Bwana. Juma Ally pamoja na Geofrey Mwipopo. Walifungua kesi dhidi ya Wajumbe wa Baraza la Wadhamini ambao ni Mama yetu Fatma Karume, Abeid Mohamed Abeid na Mzee Jabir Katundu kwa madai ya kuwa hawalitambui baraza la wadhamini la Klabu ya Young Africans SC, wakidai liliingia kwa mujibu wa Katiba ya 2010 (ambayo wanadai haijasajiliwa)”
“Pili tumegundua Juma Ally Abeid alighushi sahihi ya Club kwa kujifanya Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la Club, alighushi sahihi ya Mama Fatma Karume akidai Mwakilishi wa Mama Fatma huku Mama Fatma hajui kinachoendelea, pia alighushi sahihi ya Juma Katundu, tuligundua pia Juma Ally na Geofrey Mwaipopo sio Wanachama wa Club ya Yanga, hivyo hawakuwa na uhalali wa kisheria kusimama kujadili masuala yanayohusu masuala ya kikatiba ya Yanga”
“Club pia imegundua kuna Watu wanawatumia na wapo nyuma ya hawa Watu kuvuruga amani na tayari Club kushirikiana na Vyombo vya usalama tumeanza kuwafanyia uchunguzi walio nyuma ya hawa Watu na wakibainika wote watapelekwa mbele ya Mkutano Mkuu kama ni Wanachama na Mkutano Mkuu utachukua hatua”
No comments