Rais Joe Biden Akutwa Na Virusi Vya Covid-19
Rais Joe Biden
Rais Joe Biden wa Marekani ameambukizwa virusi vya Covid-19 na ana dalili ambazo sio kali sana, Ikulu ya Marekani ilisema.
Karine Jean-Pierre, mkuu wake wa vyombo vya habari, alisema rais wa Marekani alipewa chanjo pamoja na ile ya nyongeza.
Biden, alipimwa na kukutwa na Covid mara mbili hapo awali.
Bw Biden, 81, alionekana mapema Jumatano akiwatembelea wafuasi wa chama chake huko Las Vegas na kuzungumza katika hafla iliyokuwa imeandaliwa. Lakini alifuta hotuba ya kampeni baadaye usiku.
Ugonjwa huo unajulikana huku akikabiliwa na shinikizo kubwa la kujiondoa kwenye kinyang’anyiro cha kugombea urais kwa sababu ya umri wake.
Vyombo vya habari vya Marekani vinaripoti kwamba Kiongozi wa walio Wengi katika Seneti Chuck Schumer na Kiongozi wa walio Wengi katika Bunge Hakeem Jefferies – Wanademokrasia wawili wakuu katika Bunge la Marekani – walikutana na Bw Biden kwa faragha na nyakati tofauti na kueleza kwamba kuna wasiwasi mkubwa kuwa mgombea wake anaweza kuathiri vibaya ushindani katika Bunge na Seneti.
Bi Jean-Pierre alisema rais alipanga kujitenga nyumbani kwake huko Delaware huku akitekeleza “majukumu yake yote kikamilifu wakati huo”.
Daktari wa rais, Kevin O’Connor, alisema Bw Biden alikuwa na dalili za matatizo ya kupumua, ikiwa ni pamoja na mafua na kikohozi na alipewa dozi yake ya kwanza ya Paxlovid.
Alijisikia vizuri wakati wa hafla yake ya kwanza ya siku hiyo, lakini baadaye akapatikana kuwa na maambukizi, Dk O’Connor alisema.
Bwana Biden baadaye alitumia mtandao wa X ambao zamani ulijulikana kama Twitter kumshukuru kila mtu kwa “kumtakia mema” na akasema “atahakikisha kazi inafanyika kwa watu wa Marekani” wakati anaendelea kupona.
No comments