Mitihani ya Ujirani mwema Darasa la saba kufanyika Kila Jumamosi Miono.
Habari za Leo wana Miono tukiwa tumebakiwa na mwezi mmoja na wiki mbili vijana wetu WA la Saba kufanya mitihani Yao ya mwisho tuna mikakati tumeiweka ambapo mkakati mkubwa ni kuwakutanisha wanafunzi wote Kata nzima kufanya mitihani ya ujirani mwema kila wiki Kwa siku ya jumamosi.
Kwa nyakati tofauti tumetembelewa na VIONGOZI wetu na ndugu zetu katika kututia moyo ambapo Mh. wetu Diwani Juma Mpwipwi ametutembelea na kutupatia rim 25, na kuweka umeme WA Solar shule ya msingi Komkomba ili watoto wajisomee nyakati ZA usiku. pia brother mchama ametutembelea na kuwanunulia vitafunwa vya chai Kwa walimu wanaofanya Kazi hiyo.. tunawashkuru Sana VIONGOZI.
Ndugu
zangu sasa ni kipindi mahsusi kwa watoto wetu kwenda kutekeleza yale malengo
tunayoyadhamiria. niwaombe sana wote tushikamane kuwatia moyo na nguvu vijana
wetu ili tuje tupate ufaulu wa asilimia mia moja katika kata yetu.
Karibuni
sana kila jumamosi au mashuleni kwao kuwatia moyo watoto wetu na walimu wetu,
hata chochote utakachojaaliwa mungu atakubariki. tupambane tuinue pamoja
taaluma miono.
Ahsanteni
Sana.
No comments