Historia ya Kanisa na Kuingia Kwa Ukristo Mandera - Miono
Na Juma Hassani Kolwa (CHIEF KOLWA).
Fahamu historia ya Kanisa la mandera lilipo mkoani pwani katika kijiji cha Mandera na mto wa wami, kijiji ambacho kinapakana na vijiji jilani kama vile miono, hondogo, Makole na wami
Hapa chini anaeleza msimuliaji wetu wa mambo ya kihistoria bwana Juma Hassan Kolwa maarufu kama (CHIEF KOLWA) Ambae siku chache zilizopita alituletea historia ya dini ya kiislam ilivyoingia katika kijiji cha Miono kama hukuisoma Historia Hio basi Bofya Hapa Kuisoma Au endelea na historia hii ya ukristo na kanisa la mandera kama ifuatavyo anavyoeleza hapa chini;
Kwanza fahamu kanisa la Kwanza Tanzania Limejengwa Unguja mnamo mwaka 1860, na Kanisa la pili lilijengwa Bagamoyo miaka ya 1868.
Baada ya hapo ndipo walipoanza kueneza ukristo eneo la Africa Mashariki, Ndipo wakatumwa mapadri kununua maeneo ya misionary, Ulitumwa msafara kutoka Bagamoyo na walipofika kwa wakwere Bagamoyo walikutana na mfalme alieitwa kwa jina la Mwenepila ambae aliwafukuzwa.
Baada ya kufukuzwa bagamoyo wakaendelea na safari yao wakavuka mto wami na kabla ya kufika Mandera aliekuwa mfalme wa kijiji cha mandera aliyeitwa Sultan Shomvi Kingalu aliota ndogo ya msafara wa watu weupe, Kama kawaida Mfalme huyo aliwaita wanajimu wake ili waje wamtafsirie maana ya ile ndoto.
Wakati wamekaa na wanajimu wake, mara sultan kingaru akaanza kucheka, wanajimu wake wakamuuliza "Mkuu unatucheka" Akajibu, Hapana Nacheka lile lililonifanya niwaite, Mnaona ule msafara unaingia, Baada ya huu msafara kukutana na mtu shabab Sultan Kingaru ndio wakatoa ombi lao la kuuziwa sehemu ili wajenge kijiji chao cha misionary (Ukristo).
JIBU LA SULTAN KINGALU
Mimi sina mamlaka isipokuwa nitawapeleka kwa mfalme KOLWA wa Miono yeye ndie mwenye himaya hii yote yaani kuanzia Miono mpaka mandera iko chini ya Mfalme KOLWA
Wageni hawa walilala katika hekaru la Sultan Kingaru, walikaribishwa vizuri na walichinjiwa wanyama wakala, Baada ya kuamka asubuhi Walianza msafara kwenda kwa Mfalme KOLWA Ambae kwa kipindi hicho alikuwa yupo sehemu inayoitwa Kwedilima (kitongoji kinachopatika katika kijii cha Miono) huku Sultan Kingaru akiongoza msafara huo
baada ya msafara kufika kwa
mfalme kolwa alishuka Sultani Kingalu akapiga magoti mbele ya mfalme Kolwa na
kuzungumza lengo la wageni aliokuja nao.
wanataka kununua eneo la kijiji
ili wajenge mionary yao, Mfalme Kolwa alikubali ombi lao na akamuagiza Sultan Kingalu
(kawenge kwe mbutu) kiswahili kawape kule kweye mawe ambako ndio (Mandera) wale
mapadri walitoa pishi moja ya rupia kununua Mandera hii ilikuwa mwaka
1880.
Ilipofika 28/1/1881 ndio misa ya
kwanza kufanyika mandera.
Kijiji cha mandera ni wakristo.
na dini hii kwedilima ambako ndio kwa Mfalme Kolwa wao waliikataa na kumshauri Mfalme
kuwa watafute dini nyingine ndio walitumwa maulana Salum Kibwana Mganga Kolwa
kwenda kusoma Uislam na kuuleta miono Katika nilivyoelezea katika historia ya
uislam miono na alieuleta.
hivyo kumebakia kama ifuatavyo:
1) Miono ni waislam, NA 2) Mandera ni Wakristo na hio ndio historia fupi ya ukristo na Uislaam ulivyo ingia huku kwetu
TAARIFA ZA VIFO VYA MARAFIKI WA MAPADRI MANDERA,
Tarehe 20/05/1897 Alikufa Sultan KINGALU maeneo ya Kiwangwa Bagamoyo kwa mwanamke
na Tarehe 02/091897 Alikufa Mfalme KOLWA Kwenye Tambiko la Rafiki yake Baruti,
Pia ikumbukwe kwamba Kanisa la Mandera ni kanisa la Nne la Kikatoriki Tanzania kujengwa baada ya Lile la kwanza la Unguja, pili Bagamoyo Tatu Milima ya Nguu (Muhonda) na Nne Mandera.
Msimulizi wa history ni Juma Hassan Kolwa ((((CHIEF KOLWA))))
No comments