Miono Derby Day; Watumishi wa Sekondari washinda 3-2 kwa mbinde
Siku ya Ijumaa ya tarehe 19 July katika kijiji cha Miono kulikuwa na mechi kali iliowakutanisha watumishi wa shule za sekondari na watumishi wa shuleza msingi, Mechi ambayo ilipigwa katika kiwanja cha shule ya sekondari kikaro.
Mechi hii ilipewa hadhi ya kuitwa derby kutokana na tambo za pande zote mbili wakikwambia kuwa
Hatimaye baada ya mtanange huu kumalizika kutokana na kauli hio ya utani waliokutana na kifo ni watumishi wa shule ya msingi baada ya kukubali kipigo cha magoli matatu kwa mbili
Hata hivyo matokeo haya baadhi ya watumishi wa msingi wanalalamika na refa kuwabeba watumishi wa sekondari kwa kigezo kuwa ni Mwanafunzi wa Kikaro secondary na alilikataa gori lao la tatu hivyo ilibidi iwe suluhu ya 3-3 Lakini refa alilikataa gori lao
Mechi hii ilienda mapunziko ikiwa watumishi wa sekondari wakitangulizwa kwa kupigwa goli mbili bin sufuli dhidi ya watani wao watumishi wa shule za msingi kabla ya kusawazisha magoli hayo katika kipindi cha pili
Magoli ya watumishi wa sekondari yalipatikana kutokana na sub ya Mwaipopo ambae ndie alikuwa Man of the match siku hio baada ya kuingia aliubadirisha mchezo kwa kiasi kikubwa na kufanikisha timu yake kusawazisha na kupata gori la ushindi.
wachezaji wa sekondari kulia ni mwalimu Ngawipa kikaro secondary |
watumishi wa shule ya msingi wakitoka kifua mbele kipindi cha kwanza wakiongoza 2-0 |
watumishi wa msingi wakiwa mapunziko |
No comments