Kukaya Miono Yakabidhi Rambi Rambi TSH242,000/= Msiba wa Rajabu Hussein Omari Mboko.
Ndugu jamaa na marafiki waliokutana katika hospitali ya Temeke Jijini Dar es salaam kwaajili ya taratibu za kuuchukua mwili wa marehemu mpendwa wao kuusafirisha kwenda miono ambako ndiko atakapozikwa
Michango Ya Wana Kukaya Miono
Kama ilivyo kawaida na utaratibu wa Group la Kukaya Miono ambalo limeanzishwa na wazawa wa miono na waishio miono na hata walio nje ya miono na tanzania kwa ujumla kwa lengo la kusaidia maendeleo katika kijiji chao cha miono.
Miongoni mwa kanuni za group ni kumchangia mwana miono yeyote atakayepatwa na umauti nje ya Miono, familia itapewa mkono wa pole, Na hapa baada ya taarifa ya Msiba huu wana group walichangishana fedha na kukabidhi kwa familia kiasi cha pesa kilichopatikana kama taarifa ifuatayo kutoka kwa wana familia wakithibitisha kupokea kiasi hicho cha pesa.
Shukrani za Familia - Msiba wa Mauya (Rajabu Hussein Omari Mboko)
Kwa niaba ya Familia ya Mboko, tunatoa shukrani nyingi sana sana kwa Wana Kukaya Miono kwa kutushika mkono kufuatia msiba wa ndugu yetu Mauya. Wengi mlikuja kutufariji Temeke Hosp, Kijitonyama na Miono kwenye mazishi. Pia nathibitisha kwamba familia imepokea TZS 242,000 jana jioni kama mchango toka group hili.Mwenyezi Mungu awabariki sana Wana Kukaya na umoja huu kwa upendo na mshikamano huu. Wetu mchisampula🙏🏽🙏🏽🙏🏽
Leo imefanyika Fatiha. InshaAllah Arobaini itakuwa Ijumaa Tar 6/9/2024 na Hitma itakuwa J2 Tar 8/9/2024 (Inalaliwa Jmos Tar 7/9/2024)
Asanteni sana Wana Kukaya Miono
Mtiga O
30/07/2024
No comments