Header Ads

Header ADS

Man Kifimbo, 2T, Na Salma Queen Wafanya Kweli Zanzibar Reggae Festival, 2024

picha ya Man Kifimbo, 2T, Salma Queen Wafanya Kweli Zanzibar Reggae Festival, 2024

Na Andrew Chale, Zanzibar.

WASANII wa muziki wa Rege Man Kifimbo (Tanzani), 2T Reggae Man (Rwanda), Salma Queen (Kenya) na msanii Nast Sterling (Jamaica) wameweza kukonga nyoyo wapenzi wa muziki huo kwenye msimu wa sita wa Zanzibar Reggae Festival 2024, katika viunga vya Ngome Kongwe, Mambo Club usiku wa Agosti 9,2024.

Wasanii hao kwa nyakati tofauti wameshambulia jukwaa kwa nyimbo zao mbalimbali zenye ujumbe na kuburudisha.
picha ya 2T, afanya Kweli Zanzibar Reggae Festival, 2024

Awali Msanii Man Kifimbo alifungua pazia kwa mwaka huu na kupiga nyimbo zake kama; Nipe Tano, Nunu, Sema basi, Money Money Pesa, Usikate miti, Usinga na zingine nyingi huku msanii 2T aliwekukonga na nyimbo zake kama, Fasha, Champion Woman na nyingine nyingi.

Wasanii Salma Queen yeye aliburudisha na nyimbo kama Two face, People Rise, Mama Africa na nyingine nyingi huku Msanii Nat Sterling yeye akikonga na nyimbo kama Rasta shine na nyingine.

Salma Queen afanya Kweli Zanzibar Reggae Festival, 2024

Aidha, usiku wa leo Agosti 10, 2024, Msanii Mkongwe wa rege, Ras Gwandumi kutoka Tanzania Bara,Ras Coco (Zanzibar),Kushite, Kom Zot wanatarajia kufunga tamasha hilo kwa shoo ya aina yake.

Mwisho.

No comments

Powered by Blogger.