Huduma za NHIF zarejeshwa hospitali za Aga Khan
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeeleza kurejeshwa kwa huduma kwa wanachama wake katika Hospitali za Aga Khan, mpaka pale itakapotangazwa vinginevyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Grace Temba amesema hatua hiyo inatokana na Wizara ya Afya kuendelea na mazungumzo na Hospitali ya Aga Khan juu ya utoaji wa huduma za afya kwa wanachama wake.
NHIF ilitoa taarifa ya kusitisha utoaji wa huduma za matibabu kwa wanachama wa mfuko huo katika hospitali za Aga Khan ifikapo Agosti 13, mwaka huu ikisema maombi hayo yaliyotolewa na hospitali hiyo ni kutokana na sababu za kiuendeshaji za hospitali hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Grace Temba amesema hatua hiyo inatokana na Wizara ya Afya kuendelea na mazungumzo na Hospitali ya Aga Khan juu ya utoaji wa huduma za afya kwa wanachama wake.
“Kutokana na hayo, wanachama wa NHIF, wanaweza kuendelea kupata huduma katika vituo vya Aga Khan kwa utaratibu uliokuwepo tangu awali au kutumia vituo vingine vilivyosajiliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchi nzima,” amesema Temba.
Ameongeza kuwa “Endapo mwanachama atapata changamoto yoyote awasiliane na mfuko kupitia ofisi zake zilizoko nchi nzima pamoja na kituo cha huduma kwa wateja kinachofanya kazi saa 24 kila siku kupitia namba 199 bila malipo.”

No comments