Header Ads

Header ADS

Hospitali Ya Aga Khan Yasitisha Mkataba na NHIF kwa vituo vyake 11 kati ya 24 Nchini Tanzania

Aga Khan imesitisha mkataba NHIF kwa vituo vyake 11 kati ya 24 | “Aga Khan Yasitisha Huduma na NHIF, Wanachama Kupata Huduma katika Vituo Mbadala”.

Aga Khan imesitisha mkataba wake na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa vituo vyake 11 kati ya 24 nchini Tanzania, ikiwemo Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam, kutokana na changamoto za kiuendeshaji. Kuanzia tarehe 14 Agosti 2024, NHIF itasitisha huduma katika vituo vya Aga Khan nchini.

Hata hivyo, kuna mpango maalum kwa wajawazito wanaohudhuria kliniki katika Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam. Wale waliotimiza majuma 35 wataendelea kupata huduma hadi kujifungua, wakati wale ambao hawajatimiza majuma 35 wanashauriwa kwenda katika vituo mbadala vilivyosajiliwa na NHIF.
Aga Khan imesitisha mkataba NHIF kwa vituo vyake 11 kati ya 24
Aga Khan yavunja mkataba na NHIF kwa vituo vyake 11 kati ya 24

Kwa wagonjwa waliolazwa hadi tarehe 13 Agosti 2024, wataendelea kupata huduma katika Hospitali ya Aga Khan hadi watakapopata nafuu na kuruhusiwa. Wagonjwa wengine, wakiwemo wa kliniki za saratani na dialysis, watapata huduma katika vituo vingine vilivyosajiliwa na NHIF.

NHIF Yasitisha Huduma Kwa Wanachama Kutibiwa Katika Hospitali Ya Agakhana
Taarifa kwa Umma kutoka NHIF

Mfuko umesajili vituo vingine kama Saifee Hospital na Shifaa Pan African Hospital jijini Dar es Salaam, na pia wanachama wanaweza kupata huduma katika hospitali nyingine kubwa kama Hospitali ya Taifa Muhimbili, MOI, na JKCI. Katika mikoa mingine, NHIF imehakikisha kuna vituo mbadala vilivyosajiliwa kwa huduma za haraka


No comments

Powered by Blogger.