Stanbic Bank Yatoa Msaada wenye thamani ya TZS 30 Milioni Kikaro Sekondari Miono
Benki ya Stanbic Tanzania siku ya Jumatatu ya tarehe 23 September, 2024, ilitoa msaada wa vitu mbalimbali katika shule ya Sekondari Kikaro Iliopo katika kijiji cha Miono.
Mmoja wa Viongozi wakubwa wa Benki hio Bwana Omari Mtiga ametoa taarifa ifuatayo kupitia group la wana Kukaya Miono Kama ifuatavyo.
Leo Taasisi yetu ya Stanbic Bank imetimiza yafuatayo kwenye Shule ya Sekondari KIKARO Iliopo Miono
Viti 100
Meza 100
Matanki ya maji 4 @ Lita 5,000
Miche ya Miti 100
Ukarabati wa Madarasa 16
Ukarabati wa Ofisi ya Mkuu wa Shule
Ukarabati wa Maabara 3
Jumla ni msaada wa TZS 30 MILIONI
Pia mwaka 2022 Benki ya Stambic ilichangia vifaa tiba kwenye Kituo cha Afya Miono. Thamani TZS 10 MILIONI- Aliongeza Bwana Omari MtigaAsanteni sana Uongozi wa Kata yetu ya Miono (Mh Diwani Juma R Mpwimbwi na Viongozi wengine wote), Uongozi wa Shule (Headmaster Mr Kahabi & Mwenyekiti wa Bodi Mwajuma Mchuka), na Wana Miono kwa ujumla kwa fursa ya kuchangia
No comments