Header Ads

Header ADS

Kukaya Miono Yawafariji Wanafunzi wa Sekondari Kikaro Waliounguliwa na Bweni la wavulana

Kukaya Miono Yawafariji Wanafunzi wa Sekondari Kikaro Waliounguliwa na Bweni la wavulana
Katibu Kukaya Miono na Mjumbe wake wakati wa kukabidhi nguo za ndani kwa wanafunzi wa bweni la wavulana lililoungua kwa moto

Picha ya Mheshimiwa Diwani Siku ya tukio la moto akiwa kwenye Harakati za kuzima Moto katika bweni la wavulana shule ya sekondari kikaro bila kujali cheo chake aliwajibika kwenye zoezi hili

Video baada ya kufanikiwa kuuzima moto huo japo uliteketeza vitu mbalimbali kama magodoro, madaftari, uniform Nk.

TAARIFA TAARIFA TAARIFA TAARIFA

Kukaya Miono ilianzisha harambee Kwa ajili ya kuwafariji vijana wetu wahanga wa ajali ya moto kwenye bweni lililoungua katika shule ya sekondari KIKARO

Mwenyezi Mungu alijaalia Kwa kipindi hiki watu 39 walifanikiwa kutoa kile walichojaaliwa tukafanikiwa kupata jumla ya shilingi Laki tatu na Elfu therathini na tisa (33900/=).

Tukaulizia mahitaji ambaya bado tanahitajika tuluambiwa Bado ni mengi ila tulichagua Moja wapo ambalo litakwenda kumgusa kila mmoja
Tulifanikiwa kununua

BOXER 111 Kwa bei ya jumla kila moja *3000* Kwa hiyo zili ghalimu kiasi cha shilingi 333,000/=

UONGOZI WA KIKARO SEKONDARI
Unatoa shukrani za dhati kabisa kwa Wana Kukaya Miono wote kuonesha Moyo wa huruma na upendo kwa kuuungana na Taasisi katika kipindi hiki kigumu shule inayopitia

Walimu pamoja na wanafunzi wote wanawaombea Kwa Mwenyezi Mungu awalipe zaidi ya kile mlichotoa

Vilevile msemaji Kwa niaba ya wanafunzi pia alitoa shukrani ziwafikie Wana familia ya Kukaya Miono wote na wanaombea mzidi kuwa na Moyo wa Imani huo huo

Kukaya Miono Yawafariji Wanafunzi wa Sekondari Kikaro Waliounguliwa na Bweni la wavulana

Kukaya Miono Yawafariji Wanafunzi wa Sekondari Kikaro Waliounguliwa na Bweni la wavulana

Kukaya Miono Yawafariji Wanafunzi wa Sekondari Kikaro Waliounguliwa na Bweni la wavulana

Kukaya Miono Yawafariji Wanafunzi wa Sekondari Kikaro Waliounguliwa na Bweni la wavulana

Team ya Kukaya Miono iliambatana na wajumbe wanne

1. SADIKI MCHAMA

2. Kessy H. Othman

3. Adam Juma Nassoro

4. Mtaula Iddy Mtaula
Vilevile tuliambatana na Afisa Elimu Kata ya Miono

Mwl. Dibwa Juma Dibwa

Ahsanteni Mungu atubariki Sote.

Sadiki Mchama
Katibu -- Kukaya Miono

4/11/2024

No comments

Powered by Blogger.